Tunachokifanya

Kwa miaka 20 ya utendaji kazi wake, KISEDET  imeanzisha na kuendeleza miradi mingi. Baadhi ya hiyo imeisha, mingine imeimarishwa na kendelezwa kwa sababu imebeba malengo makuu ya Shirika, na imeshikiria dhamira ya shirika linavyofanya kazi.

Katika miradi yote hii kuna watu wengi waliohusika na mawazo mengi yalizingatiwa mpaka kutufikisha hapa tulipo.

Sisi kama wanachama wa shirika, viongozi na tumu nzima ya wasimamizi, hatutapoteza ndoto na malengo yetu kwa sababu ya changamoto mbalimbali tunazozipitia. Kufanya kazi na/pamoja  watu ni ngumu, lakini kwa miaka yote hiyo malengo yetu yamedhihirishwa kikamilifu kwa kazi nzuri zilizofanywa, sio kwa kutoa njia/kutatua matatizo yao haraka ila ni kuwapatia watu zana bora za kuwasaidia kuwa na maisha bora.

Katika miradi yote tuliyoitekeleza, kama KISEDET tumefanya tathimini na kujaribu kujifunza kulingana na changamoto na mafanikio tuliyoyapata.

Tunatumaini kuwa tuna miaka mingi inayokuja na kujifunza, shukurani za kipekee kwa wote wanaoendelea kushirikiana nasi na kutusaidia.