Kuhusu Sisi

Tunaona fahari kufanya kazi na watoto. Kazi za kifamilia zinatufanya tukutane na watoto ambao wapo katika mazingira duni na wenye uhitaji wa makazi, kutunzwa, wanaohitaji ushauri na nasaha, kulindwa, afya, elimu na mafunzo ya ufundi/ujuzi pamoja na kuunganishwa na familia zao. Tumejidhatiti kuwahudumia/kuwasaidia watoto.

Tunawasaidia watoto kuondokana na mazingira hatalishi. Kuwasaidia kutimiza ndoto zao pamoja na kuwatengenezea mahusiano mazuri baina yao na familia zao. Kwa wale wanaotaka kutafuta ndugu zao, tunawasaidia kufuatilia na kutafuta ndugu zao ili watoto hawa waweze kuunganishwa na familia zao walikotokea/zaliwa. Hii ndio KISEDET.

TAARIFA ZA SHIRIKA.

Kigwe Social Economic Development and Training (KISEDET) ilianza shughuli zake 1998 katika kijiji cha Kigwe na lilisajiliwa 18/2/1999 chini ya Trustee Incoparation Ordinance (cap 375) kama shirika lisilokuwa la kiserikali, lisilo la kibiashara na lisilo la kisiasa. Januari 2006 katiba ya KISEDET ilibadirishwa na tangu May 7, 2007 lilisajiliwa kama shirika/asasi ya kiraia chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2020 lenye namba ya usajili 1802.

KISEDET  inafanya kazi zake Tanzania bara, na tangu kuanziashwa kwake limejikita/kulenga shughuli zake katika mikoa ya Dodoma na Singida.

KISEDET inalenga kuwawezesha watoto na jamii yenye uhitaji waweza kupata elimu na kuwajengea uwezo ili wautumie kupunguza umasikini.

Utume wa shirika ni kuwasaidia watoto wanaotoka katika familia duni wanaoishi Dodoma na Singida, kwa kutekeleza shughuli zinarandana na elimu na kuboresha hali za watu na kuwasaidia vijana na watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wapate elimu na ujuzi wa kimaendeleo.

Shirika lina bodi ya wakurugenzi inayojumuisha wajumbe 7 (2 wanawake) ambao hukutana mara moja kila baada ya robo ya mwaka, na lina wafanyakazi 31 (8 wanawake). Kwa sasa shirika lina vituo viwili vya kulelea watoto kimoja kipo Dodoma mjini (Shukurani) na kingine kipo nje kidogo ya mji (Chigongwe), 25km kutoka mjini. Mbali na hivyo, KISEDET lina kituo cha kutwa kinachotumika kama sehemu ya kuingilia na kusajilia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kwenda kwenye makao.

Shirika lina Malengo na mikakati ifuatayo:

  1. Kuwaunganisha watoto na familia zao kupitia mbinu mbalimbali zilizowekwa.
  2. Kuwa mawakili na kutoa semina mbalimbali juu ya afya katika familia na VVU/UKIMWI, haki za watoto, unyanyasaji majumbani na ukatili dhidi ya watoto, vijana na watoa huduma.
  3. Kufanya kazi na jamii ili kuhamasisha na kuwawezesha kiuchumi vijana na wazazi kupitia VSLA.
  4. Kuwatengeneza na kuwabadilisha watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
  5. Kuhamasisha na kufanya kilimo kipya endelevu kwa kuanzisha kilimo rafiki kwa mazingira na kudhibiti maji.
  6. Kuwaelimisha na kuwashauri vijana na jamii juu ya maambukizi ya VVU/UKIMWI, kuzuia na kuwatunza watu wenye maambukizi.
  7. Kuhamasisha na kutunza mazingira kwa afya bora, ukuwaji wa uchumi na kupunguza umasikini.
  8. Kuwasaidia watoto wa mitaani, yatima, wazee wasiojiweza, watu wenye ulemavu na watu maskini/duni zaidi.
  9. Kulinda, kutetea na kutekeleza sera ya ulinzi na usalama wa mtoto, wafanyakazi na wazee wasiojiweza pamoja na kulinda maisha yao.
  10. Kusaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kijamii kama vile shule, vyuo vya ufundi na vituo vya afya.

Ulipaji wa Ada za shule kwa wanafunzi wanaosoma shule binafsi.

Shirika lina utaratibu wa kuwalipia ada watoto wanaosoma shule binafsi pamoja na vyuo vya ufundi na vyuo vikuu.

Kutoa mitaji ya kibiashara kwa wazazi ambao watoto wao wapo kwenye mradi ili kuwawezesha kiuchumi.

Shirika pia lilitenga fedha kuwawezesha kiuchumi wazazi wenye watoto kwenye mradi wetu lengo kubwa likiwa ni wazazi wajishughulishe katika shughuli za uzalishaji mali kwa kuanzisha vikundi vya kukopeshana ili kukuza kipato chao na kuweza kuwasaidia watoto wao na jamii inayowazunguka. Mpaka sasa zaidi ya wazazi 150 wamenufaika na mradi huu. Mradi huu unaojulikana kama “mradi wa vikundi” unafanya kazi katika maeneo ya Chigongwe ambapo kuna wanachama zaidi ya 77 na Itigi (Singida) wanachama zaidi ya 90 wote wakiwa ni wazazi.

Ujenzi wa miundombinu ya shule.

Shirika lilianzisha mpango wa kuboresha na kujenga miundombinu ya elimu(shule) kulingana na bajeti tunayoipata kutoka kwa wafadhili. Mpaka kufikia 2020 shirika limeweza kukarabati majengo mawili na kujenga darasa moja la shule ya msingi Bangayega.