Help street children in Tanzania

Home>Habari>Uncategorized>Vikundi Vya Ujasiliamali

Kuinua kiwango cha maisha kwa wazazi wenye kipato cha chini.

KISEDET imerithi msemo wa Nyerere baba wa Taifa, wakati tunaanzisha mradi wa kijasiriamali tukilenga familia za Itigi (mkoa wa Singida) na Chigongwe (mkoa Dodoma).

‘Huwezi kuwaendeleza watu. Waruhusu watu wajiendeleze wenyewe’.

Baaada ya utekelezaji wa awali na mafunzo yaliyofanywa na wataalam wetu, KISEDET ilijihusisha kutoa mtaji katika mradi huu kwa watu waliokuwa tayari kujiunga katika vikundi ili waweze kukopa na kurudisha kwa riba ndogo kwa ajili ya kuinua shughuli zao za kiuchumi au kuanzisha nyingine.

Kwa njia hiyo, watu wanaanza kujitegemea wenyewe na kuanza kusaidia familia zao kuliko kutegemea misaada kutoka njee lakini zaidi ya yote kupata utu ambao kula mwanadamu huupata kupitia kazi. Kisedet tunaamini kuwa kutoa misaada sio njia peke ya kusaidia watu.

Kwa mwaka huu sare zote za shule zilishonwa na kikundi cha mafundi cherehani wa Itigi ambapo ni njia nzuri ya kuwaingizia kipato na kukuza uchumi wao.

Kati ya 2018 na 2019, Kisedet ilitoa mitaji ya kianzio yenye thamani ya Tsh 4.5 milioni kwa kikundi cha wazazi Itigi na 4.0 milioni kwa kikundi cha wazazi cha Chigongwe (MKICHI). Vikundi hivi vimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuzungusha fedha hizo. Kwa mfano, kikundi cha wazazi Itigi kina jumla ya wanachama zaidi ya 77 (55 wanawake), ambapo wamezungusha mtaji wao zaidi yamara sita. Wameweza kukopeshana mpaka kufika kiasi cha Tsh. 30,295,000. Ambapo kwa Chigongwe wameweza kuzungusha zaidi ya mara nne na jumla ya mikopo iliyotolewa  ni Tsh. 17,870,000 kwa wanachama 63. Mradi huu unamalengo ya kukuza hali za kiuchumi za wazazi wenye kipato cha chini kupitia huduma ya kifedha katika vikundi kwa kuwekeza katika biashara ndogondogo kwa maisha bora kwa binafsi na kwa familia zao.

Utekelezwaji wa mradi huu unafadhiliwa na shirika la “Agata Smerlada Florence”.