Michango yako kwenye kazi zetu itatusaidia kutambua mahitaji muhimu zaidi ya watoto wa mitaani tunaowahudumia. Kwa mchango wako mdogo unaweza kutusaidia kujenga darasa zima, miradi mingine tuliyonayo ya watoto na kusaidia kituo cha watoto cha shukurani kinachomilikiwa na Kisedet.
Ths 30,000/= kwa mwezi
Kwa mchango wa kila mwezi, utasaidia mtoto mmoja kupata mlo mzuri kwa siku
Tsh. 50,400/= mchango wa mara mmoja
Kwa mchango mmoja wa Tsh. 50,400 utakuwa umemsaidia mtoto/kijana anayeishi na kufanya kazi mtaani, kupata bima ya afya ya NHIF kwa mwaka mmoja au utakuwa umemsaidia kuhudhuria Makao ya kutwa kwa wiki mbili. Hivyo ataweza kuoga, kufua nguo zake, kupata mlo mmoja wa chakula, na kuhudhuria vipindi mbalimbali.
Tsh. 150,000/= mchango wa mara mmoja
Kwa mchango mmoja, utamsaidia mtoto/kijana anayeishi na kufanya kazi mtaani, kuweza kuhudhuria Makao yetu ya kutwa kwa mwezi mmoja. Kwa mazingira haya salama na kwa msaada wa maafisa ustawi wetu, mtoto/kijana huyu ataanza hatua za kuunganishwa na jamii/ndugu zake.
Tsh 200,000/= mchango wa mara mmoja
Kwa kuchangia Tsh. 200,000/=, mtoto/kijana anayeishi na kufanya kazi mtaani atatunzwa kwenye makao yetu ya muda mrefu “Chigongwe family”, kwa muda wa miezi wili, kwa kuongezea, utakuwa umesaidia pia kuandikiswa kwenye shule za serikali na kukatiwa bima za afya.
Haya ni mifano tu, mtu anaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha! Shukurani za dhati!
Kama utahitaji kuwa mfadhili au kusaidia gharama za elimu kwa watoto au kwa kwa kazi yoyote inayofanywa na KISEDET, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:
info@kisedet.org au piga: 0738/143273
Kwa kuchangia kupitia Benki:
KISEDET-KIGWE SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT
ABSA BANK TANZANIA LIMITED
BANK CODE: 020
TAWI LA DODOMA
MSIMBO WA TAWI: 008
NAMBARI: 0086002000
MSIMBO MWEPESI: BARCTZTZ
M-PESA 0760 862975 Kigwe Social Economic Development & Training
Unapoguswa tafadhali changia kiasi chochote ulichonacho. “Ndondondo si chururu”
