Wadau wetu

Washirika wetu wa thamani (wa zamani na wa sasa), na vyanzo vya fedha ni: 

Gruppo Tanzania Ets Ni shirika  “Dada” kwetu nchini Italia, lililopo katika mkoa wa Lombardia, Kaskazini mwa Italia. Wanachama wake wanatoka Mikoa tofauti. Iilianzishwa ili kusaidia, kukusanya fedha na kukuza shughuli za Kisedet nchini Italia. Ni chanzo kikuu cha fedha kwa KISEDET. 

Progetto Agata Smeralda  liko Florence, Tuscany, katikati ya Italia. Waliunga mkono kuchimbwa kwa kisima katika makao ya watoto ya Chigongwe, basi dogo, mradi wa OVC huko Itigi, Mkoa wa Singida, na mradi wa mikopo midogo. 

Kanisa la Waldesian. Tangu mwanzoni mwa mwaka 2023, Shirika lisilo la Kiserikali la Kisedet limepokea mchango wa 8×1000 kutoka Kanisa la Waldensian kwa ajili ya utekelezaji wa miradi tofautitofauti. 

USAID/PACT na Railway Children Africa ni wadau wa KISEDET katika mradi wa Kizazi Kipya.

Maria Centro Donna Marafiki zetu wanawake kutoka mkoa wa Lombardia Kaskazini mwa Italia, waliiunga mkono KISEDET hasa katika ujenzi wa nyumba ya watoto ya Chigongwe; walijenga nyumba ndogo ya kwanza (sasa ni ofisi).

IPSOS FOUNDATION walikuwa washirika wa Kisedet katika mradi wa EDEN

UN walikuwa washirika wa Kisedet katika mradi wa FURSA

Arcobaleno su Tanzania Ni muunganiko wa waitaliano kutoka mikoa ya Gallipoli na Puglia kusini mwa Italia. Wanaisaidia KISEDET katika shughuli nyingi ikiwemo ujenzi wa kituo cha makao ya watoto Chigongwe, na pia wanasaidia uchimbaji wa bwawa la kufugia samaki.

  •  

Shukrani za pekee kwa Banca Barclays, Shirika la Bima la Zanzibar, na watu binafsi kwa kutuunga mkono kwa njia nyingi tofautitofauti.

  •