MRADI WA WISE: 8×1000 Kanisa la Waldesian

Mradi wa WISE unalenga kuboresha uwezo wa shirika kuendelea kutekeleza shughuli zinazoruhusu watoto wenye umri kuanzia miaka 4 mpaka 14, wanaoishi katika makazi ya muda mfupi ya Shukurani, au wale wanaoenda katika kituo cha mapokezi cha mchana (drop-in centre), kurudishwa katika makazi yao na baadae kuishi na familia zao baada ya kuunda mazingira salama kwa ajili yao.


Watoto walioletwa kwetu kwa kupitia ziara za uhamasishaji mitaani au kuletwa KISEDET na Ustawi wa jamii au polisi, wanaanza kuishi katika makao ya muda mfupi ya Shukurani. Baadhi ya wasichana, huletwa katika makao yetu kwa sababu walikuwa wakifanyakazi za ndani (house girl) na kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili. Pia walikuwa wanapewa kazi nyingi sana kama kupika, kufua, kunyoosha nguo, kulea watoto, nk…Wasichana hawa wanaishi kama watumwa.
Watoto hawa wanahitaji msaada wa kisaikolojia na kijamii ili kufafanua sababu zilizowasababisha wapitie ukatili huo ambao umewasogeza mbali na familia zao na kuenda katika maisha ya mitaani na hapa ndipo mradi wetu unaingilia kati. Vikao kadhaa vinahitajika mpaka waanze kusimulia hadithi zao na tuanze kutafuta wazazi na familia zao.
Ziara za familia pia ni muhimu ili kuwafundisha umuhimu wa elimu na haki za watoto kupitia semina kuhusu malezi. Mradi huo ni kati ya program ya umuhimu sana ulioanzishwa na KISEDET mwaka 2019 mpaka 2023 ambao unalenga kusaidia watoto 2,400 wanaoishi katika mazingira magumu ifikapo mwaka 2023.
Program hio inajumuisha shughuli mbalimbali kama: kutoa mahitaji ya msingi kwa watoto katika vituo vya mapokezi, kuandaa siku na ziara usiku kwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ili kuwaelekeza katika makao yetu ya mapokezi, kwa kupitia shughuli za michezo, kuwasaidia katika uandikishaji shuleni na kujaribu kufuatilia familia na kuhakikisha kwamba watoto wanaweza kurudishwa kwao.
Mradi unajitahidi kufafanua haswa hatua ya mwisho kati ya hatua hizi na watoto waliochaguliwa ni watoto 40 wenye umri kati ya miaka 4 hadi 14, ambapo 25 wanaishi ndani ya makazi ya mapokezi ya muda mfupi inaoitwa Shukurani na 15 wanaishi nje na kuhudhuria kituo cha mchana. Malengo ni kuhakikisha watoto wako vizuri kisaikolojia na kuwafundisha wazazi au familia zao juu ya malezi. Ili kuweza kufikia malengo haya yatimie, mtaalamu wa kisaikolojia anayefanya kazi na watoto na mtu wa ustawi wa jamii ambaye ana jukumu la kufuatilia familia na kufanya ziara kwa wanafamilia wanahitajika.
Katika miezi miwili ya kwanza ya mradi (ilioanza tarehe 1 Januari 2024), tahadhari itaelekezwa kwenye utafiti wa familia na msaada wa kisaikolojia kwa watoto ambao tayari wanaishi katika kituo cha mapokezi cha Shukurani.
Kuanzia mwezi wa tatu, ziara zitafanyika kwa wanafamilia mpaka patakapo itajika na zitaweza kutokea mara kwa mara kulingana na umbali kutoka kwa makao makuu ya KISEDET, au zitafanyika kwa kupitia simu manaake asilimia kubwa ya watoto hawa wanatoka mikoa ya mbali. Msaada wa kisaikolojia pia utakuwa kipaumbele na utaendelea hadi wakati wa kuungana tena na familia zao, mara moja au mbili kwa wiki kulingana na ukatili waliyo pitia.
Kwenye mwezi wa nne wa mradi, walengwa wa kwanza wataungana na familia zao tukishaona kwamba wanautulivu wa kisaikolojia na hamu ya kurejea nyumbani kwao, pia tunaangalia utayari wa familia kuwatunza na uboreshaji wa tabia kuelekea kwa mtoto. Umaskini umeenea na mara nyingi ndio chanzo kikuu cha kutoroka shule na nyumba.
Hata hivyo, matatizo ya kiuchumi ya wazazi hayawezi kuwakilisha kikomo cha kuungana tena ikiwa hali zingine kama vile upendo na ulezi bora utatumika, ndiyo maana mchakato wa ujumuishaji pia hutoa usaidizi wa kifedha kusaidia shughuli ndogo za kibiashara ambazo tayari zimeanzishwa katika familia ili kuwaruhusu kuwa huru zaidi.
Baada ya kurudishwa pamoja, angalau ziara moja ya familia pia imehakikishwa kwa kila mtoto, kuangalia hali ya mtoto nyumbani, maendeleo yake shuleni na hatua zozote muhimu zaidi.
Tunalishukuru kanisa la Valdesi kwa kuipa KISEDET fursa ya kuendelea na moja ya miradi muhimu na kuwahakikishia mshahara wafanyakazi wetu wawili ambao wanaruhusu haya yote kuwezekana kwa kujitolea kila siku.

Afisa ustawi wa KISEDET Hamisi Ndoje katika kipindi chake cha mitaani, cha kukutana na kutoa ushauri kwa vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Maafisa Ustawi wa KISEDET, Hamisi Ndoje na Mtahu Muhibu, wakati wanapokuwa kazini mitaani kwa ajili ya kukutana na watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mitaani.