UCS 2023/24: miezi minne tangu walipoingia Tanzania

Imeshapita miezi minne, tangu Mradi wa UCS ulianza. Mradi unalenga kuwaunganisha watoto na familia zao. Hapa chini UCS wametoa mawazo yao kuhusu uwepo wao katika kipindi hiki.

DAVIDE: Tarehe 4/02/2024, miezi 4 tayari imepita tangu nimeanza experience yangu na Universal Civil Service (UCS). Wakati ninawaza kuhusu miezi yiliopita, ninahisi kama vile tuliondoka jana, lakini kwa wakati
huo huo ni kama muda mrefu zaidi umepita, kwa sababu ya kazi nyingi, matukio na uzungukaji wengi uliofanyika katika miezi hii ya kwanza nchini Tanzania. Nitajaribu kukuelezea kile ambacho nimepitia katika miezi iliyopita kwa kutumia maneno 4: Oktoba, UGUNDUZI. Mwezi wa kwanza ulikuwa wa ugunduzi, wa hamu ya kujifunza zaidi kuhusu maisha haya mapya, kuzoea midundo ya maisha ya Kitanzania lakini kwa wakati huo huo kuishi kila siku
kiutulivu, kufahamiana na wenzako ambao watakuwa marafiki na wafanyakazi wenzako kwa mwaka mzima. Novemba, ADAPTATION. Sifa hii inahitajika Dodoma. Mwezi huu wapili ni mwezi ambao tulianza kufahamu jiji la Dodoma, tukazoea lugha, chakula, kazi na kujituma kadri tuwezavyo kuleta msaada wetu kwa KISEDET na Gruppo Tanzania. Desemba, SHUKRANI. Mwezi wa mwisho wa mwaka 2023 ulikuwa wa furaha zaidi. Nilikumbuka jinsi nilivyoshukuru kwa kuumaliza mwaka katika nchi nyingine kwa mara ya kwanza, jinsi ninavyoshukuru
shirika kwa kunichagua, kwa watu wote niliokutana nao katika ‘safari’; hii na watoto kwa tabasamu lao ambalo, atakama wamepitia maisha magumu, kwa sababu ya Kisedet wameweza kutabasamu tena na
kututia moyo kila siku. Januari, HAMASISHA. Mwezi wa kwanza wa 2024 ulikuwa mwanzo wa miradi na changamoto nyingi mpya, motisha na dhamira ya kuendeleza experience hii kwa ukamilifu na kusaidia miradi ambayo KISEDET wanasimamia, sio tu katika makao ya KISEDET lakini pia katika mikopo midogo midogo, darasa la watoto walemavu, shule za kitaaluma na mengi zaidi.
Ninabeba nami mafunzo na experience ambayo watu walio karibu nami wamenipitishia, na ninaendelea kuimarisha mzigo wangu wa kihisia na kitaaluma.

AGNESE: Uzoefu wangu wa Huduma za kiraia kimataifa (UCS) na Shirika lisilo la kiserikali la KISEDET ulianza tarehe 4 Oktoba mwaka 2023. Nilipotua Dodoma, pamoja na wenzangu, nilitawaliwa na mawazo mengi na mihemko ambayo ni ngumu kuelezea. Niliendelea kujiambia “Hii si safari tu; itakuwa nyumba yangu kwa mwaka moja.” Nilihisi furaha kubwa nilivyofika na pia hofu ambayo ni sifa ya kila mtu na hamu nilivyogundua vile ambavyo vinaningoja.
Miezi minne sasa imepita, na nimejiskia kwamba nimekaribishwa na kufuatiliwa kiukaribu na
OLP (msimamizi wa mradi) wetu Gio, waendeshaji wote wa KISEDET na watoto katika
makao ya Kisedet. Shughuli ambazo sisi UCS tunafanya zinatofautiana sana na hii inaturuhusu kufahamiana na miradi yote ya Shirika. Na pia, kazi zinazofanywa zinafanyika kwa ushirikiano na msaada wa wafanyakazi wa KISEDET. Hii inaruhusu tubadilishane mawazo na ushauri. Wakati nipo katika makazi ya muda mfupi “Shukurani” shughuli ninazofanya ni kuandaa post kwenye social media, kuandaa faili au nyaraka, kuweka lebo kwenye bidhaa za duka la mshikamano na kuandaa shughuli/michezo kwa watoto wa makao hayo. Katika makazi ya muda mrefu ya “Familia ya Chigongwe”, pia nina fursa ya kufanya kazi mbalimbali nje, kwasababu kuna eneo kubwa ambalo lina bustani ya mboga na matunda, kitalu na banda la kuku. Hata hivyo, changamoto hazikosekani kama vile lugha, lakini hii pia inanisisimua na kuniruhusu kushiriki. Ninashukuru kuishi tukio hili kwa sababu ninapata fursa ya kufahamu utamaduni tofauti, watu wenye tabia tofauti na ningependa kujaribu kuelewa mambo mengi zaidi. Nikijaribu kuelezea miezi hii michache ya kwanza, ningetumia usemi “kubadilishana maoni” ambayo labda wakati wakuondoka itabadilika kuwa “kubadilishana mawazo”. Sijisikii kama “mimi ni mtu mzuri”, sitaki kubadilisha dunia, au Tanzania, au Kisedet au maisha ya mtu yeyote hapa; Ninataka tu kutazama, kujumuisha na kuchangia, ambavyo naamini kwamba ndo vitu vya thamani zaidi.

SIMONE: Nilianza experience yangu na United Civil Service (UCS) kwa ajili ya ukuaji wangu binafsina nilitaka kutafuta sehemu amabayo ina mawazo na maadili kama yangu. Baada ya kutafuta kwa muda mrefu, nilipata mradi wa KISEDET ambao ulinishangaza katika shughuli mbalimbali na dhamira wanazofanya na ushirikano na nilijiskia kwamba nilikuwa nakubaliana nazo kabisa.
NilifikaTanzania kwa kiumakini sana, nikijaribu kutazama kadri niwezavyo bila kuhukumu na kujiruhusu kujipoteza na yale niliokuwa naona. Nilikuwa najiskia nimevamiwa na kila kitu nilichokua naona na macho hayakuacha kutazama na akili haikuacha kusindika habari.
Tangu mwanzoni, wanfanyakazi wenzetu na watoto walitukaribisha kwa furaha na tulishirikishwa katika shughuli mbalimbali kazini. Pia walituruhusu kutembelea jiji na kutufafanulia tabia na desturi za Kitanzania.
Ninaamini ni muhimu sana kwetu kushirikiana kila siku na wafanyikazi wa ndani kwa sababu inaturuhusu kuexchange mawazo na uzoefu tofauti na kujifunza kutoka kila mtu. Kazi zetu hapa ni mbalimbali (kutunza bustani, shughuli na watoto na kazi za ofisini) na hii inanichangamsha sana.
Baada ya miezi hii 4 ya mwanzo naweza kusema nimejifunza mengi na natumaini pia nimetoa mchango wangu mdogo. Kuna mambo ambayo bado sielewi na ambayo labda sitayaelewa na mengine ambayo nataka kuondoka nao.

ELISA: Nilichagua UCS (Huduma za kiraia kimataifa) bila mawazo sana na ninashukuru kwamba sijaendelea kuwaza sana na nimesafiri tu kwa sababu baada ya miezi mitatu, sijawai kuwa na furaha sana. Niliondoka Italia bila matarajio, nikiwa na hamu ya kufahamiana na utamaduni mpya bila ubaguzi na hamu kubwa ya kujifunza: Nilitamani kujifunza njia tofauti ya kuishi na kurudi na ujuzi huu Italia. Nilijifunza kuhusu UCS kutoka kwarafiki yangu. Kisha nilitafuta shirika ambalo lilikuwa na mizizi katika eneo hilo na kuheshimu utamaduni wa mahali hapo na ndipo nilipopata KISEDET: shirika ambalo lilionekana kuwa kidogo, lakini kwa kweli limesaidia watoto na familia nyingi zilizo katika hali tete. Nilikuwa na hofu nilivyoshuka katika uwanja wa ndege: “Je, hapa patakuwa nyumbani kwangu? Kweli? Kwa mwaka mzima? Eti nitajifunzaje lugha? Je, nitaweza kufahamiana na watu?’ Nilihisi kuchanganyikiwa, lakini hisia hii ilipotea haraka tu nilipogundua ukarimu wa KISEDET na Tanzania. Uzoefu wetu wa UCS ulianzia ‘Shukurani’, makazi ya muda mfupi ambayo pia makao ya kutwa (Drop-in Center) ipo na inapatikana jijini Dodoma. Wafanyakazi walitusaidia kuzoea maisha haya hatua kwa hatua kwa kutuunga mkono na kutusaidia katika kazi yetu ya kila siku: nadhani njia hii ilikuwa ya msingi ili tuweze kuelewa mazingira kabla ya kuanza kufanya kazi kwa bidii.
Baada ya miezi miwili, tulihamia kijiji cha Chigongwe (ambacho kiko kilomita 30 kutoka Dodoma), na ndipo makazi ya muda mrefu ya ‘Familia ya Chigongwe’ yanapatikana: hapa tuligundua aina nyingine ya maisha. Na baada ya muda mfupi pakawa nyumbani kwetu.
Na sasa baada ya miezi minne hapa, ninahisi kama nimepata utulivu na maelewano pia, lakini najua
kwamba bado kuna mengi ya kugundua na mda amabao tunao hapa hautakuwa wa kutosha. Nadhani
kwamba ili kujiskia vizuri katika uzoefu huu ni muhimu kujifungua na kusikiliza, kuondoa ubaguzi wa aina
yoyote: ni muhimu pia kuelewa ni nini kinachotofautisha na kupingana na njia yetu ya maisha.
Ninawashukuru UCS na Tanzania kwa sababu waliniruhusu kugundua utamaduni mpya na kuufahamu vizuri zaidi.