Ufadhili

Watoto wote wana haki sawa haijalishi wanaishi nchi gani. Katika nchi tajiri za magharibi, wazazi wanajitahidi kuwafanya watoto wao wasiwe wanene (wakiwa na mitazamo hasi juu ya afya zao), Tanzania, asilimia kubwa ya watoto wanakula mlo mmoja kwa siku, bidha na huduma ambazo kwa nchi nyingi wanachukuli kama mahitaji muhimu (mavazi, elimu nk) kwa baadhi ya watoto hawa imebaki kuwa ndoto.

Baadhi ya watoto wana sare za shule na nguo za jumapili tu! Tuwafanye watoto hawa ndoto zao zitimie- ni sehemu ya haki zao. Kiasi chaTsh. 200,000.00 tu yatafanya yote hayo yawezekane kwa mtoto wa kiTanzania na atakukumbuka daima.

Pia utakuwa umesaidia gharama za mesomo kwa mtoto na kijana anayesaidiwa na Kisedet, akiishi kwenye familia yake au kwenye makao ya shirika. Utamsaidia mvulana au msichana kupata mahitaji yote ya shule, kuandikisha kwenye shule za Tanzania na kugaramikia bima za afya lakini zaidi ya yote utakuwa umemsaidia zana bora za kukulia na kujenga maisha bora akiwa kwao

Hatua ya kwanza ya kumfanya mtoto aweze kutuamini na kuanza kuacha maisha ya mitaani:

Ukichangia Tsh. 100,000/= utakuwa umemfanya mtoto aweze kuhudhuria Drop In Center (makao ya kufikia) kwa mwezi mmoja akiwa anapata huduma wa kuoga, kuhudhuria vipindi mbalimbali na mlo mmoja kwa siku

Maisha Mapya

Kwa kuchangia Tsh. 250,000 kila mwaka utakuwa umeruhusu watoto wa mitaani kukaribishwa kwenye makao ya shirika la Kisedet, utakuwa umewasaidia kuishi katika sehemu salama na yenye amani na kwa msaada wa maafisa wetu watoto watakuwa wameanza maisha mapya.

Maisha ya baadae

Kwa ufadhili wa Tsh. 500,000 utakuwa umegharamikia gharama za masomo ya mtoto na kijana anayesaidiwa na Kisedet haijalishi atakuwa anaishi kwenye familia yake au kwenye makao yetu. Utamsaidia kupata mahitaji yote ya shule, kuandikishwa kwenye shule za Tanzania au katika VTC.
Nani yuko tayari kuwasiliana na kuikubali miradi yetu? Kama utahitaji kuwa mfadhili au kusaidia gharama za elimu kwa watoto au kwa kwa kazi yoyote inayofanywa na KISEDET, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:

info@kisedet.org

au unaweza kuchangia moja kwa moja Tanzania kupitia Benki:

KISEDET-KIGWE SOCIAL ECONOMIC DEVELOPMENT AND TRAINING

BENKI :CRDB

TAWI LA CHAMWINO DODOMA

KWA WAGENI WALIO NJEE YA NCHI A/C 1952447960600 (kwa euro tu)

WALIO TANZANIA A/C 0150447960600

SWIFT CODE: CORUTZTZ

Lipa kwa simu, mitandao yote na benk kupitia namba 5590401. KISEDET.