Makao Ya Kutwa

Kwa muda sasa, KISEDET imeweza kuwa na makao ya kupokelea watoto wa mitaani. (Drop in Center) inayowalenga watoto wa mitaani.

Lengo la mradi huu ni kuwakaribisha na kuwapa nafasi ya kuoga na kufua nguo zao, kuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia, kupata chakula na kuwarudisha katika mazingira halisi kupitia michezo nk

photo © Romina Remigio

Kituo kinafunguliwa kila siku kuanzia 8:00 asubuhi hadi 16:00 jioni na kama mmojawapo ni mgonjwa basi atalala hapo  usiku pia.

Wanapokuwepo hapo hujishughulisha na shughuli mbalimbali kwa kushirikiana na maafisa ustawi/wafanyakazi wetu kama vile kuchora, kazi za bustani, Yoga na tafakari, msaada wa kiushauri na kisheria na shughuli nyinginezo. Wanasisitizwa kuzingatia usafi binafsi, kusafisha mazingira ya kituo na kufuata ushauri na majukumu wanayopewa kila siku.

Baada ya mwezi ni rahisi kujua ni yupi yuko tayari kuachana na maisha ya mitaani na kuja kuishi kwenye kituo cha makao ya muda mfupi “Shukurani” na kuendelea na hatua nyingine. Kwa wale wote ambao wanakuwa bado hawako tayari, kama watapenda wanaweza kuendelea kuja na kuhudhuria Drop in Center. Milango siku zote ipo wazi kwa ajili yao. Mtu peke aliyeelimika ni yule aliyeelimishwa namna ya kujifunza na kubadilika. _Carl rogers.